• Fri. Jul 5th, 2024

Kenyan Top Stories

Telling Kenyan Stories

Wakenya Wampa Ruto C +

Byadmin

Jul 13, 2023

NA JAMES MUTUA

Mkurugenzi Mtendaji wa Trends and Insights for Africa Dkt Tom Wolf Akitoa ripoti ya utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza mapema hivi leo katika hoteli moja hapa jijini Nairobi.

Wakenya walioshiriki katika utafiti wa TIFA wa hivi karibuni wamempa rais Ruto alama ya C+ kulingana na hisia zao kuhusu ahadi zake za kampeni ya mwaka jana.

Utafiti huo uliotolewa alhamisi katika hoteli moja hapa jijini Nairobi umetoa taswira mbaya ya utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza.

Alama ya C+: Asilimia 56 inaamini Nchi ya Kenya inaelekea pabaya.

Ripoti ya uchunguzi huo ilifanyika kati ya Juni 24, 2023, na Juni 30, 2023, kwa njia ya mahojiano ya Simu iliyosaidiwa na Kompyuta (CATI) na iliwahusisha wahojiwa 1,530.

Utafiti huo ulihusisha maoni kuhusu mwelekeo wa nchi na utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza tangu ilipochukua hatamu ya uongozi miezi 10 iliyopita. Kulingana na TIFA, idadi kubwa ya Wakenya (56%) wanaamini kuwa nchi inaelekea pabaya.

Mwelekeo ambao Kenya inaelekea: Kulingana na ripoti ya Machi hadi Juni 2023

Ukusanyaji wa takwimu za utafiti ulihitimishwa kabla ya vifungu mbalimbali vya Bajeti mpya kuanza kutumika.
Wakenya wachache wanazingatia mwelekeo wa sasa wa nchi kuwa mzuri (25%), wakiwa na maelezo chache kuhusu sababu zao, huku idadi ndogo ya walio wengi (24%) wakitaja uongozi wa serikali ya Ruto kuwa sababu kuu ya kuwa na msimamo mzuri.

Serikali ya Rais Ruto: Mafanikio Makuu na Mapungufu.

Bila kujali mlengo wao za kisiasa, idadi kubwa ya Wakenya ambao wanaona kuwa nchi inaelekea pabaya, walitaja gharama ya maisha inayoongezeka kila mara.

Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *